Tume inayosimamia utekelezaji wa katiba mpya nchini Kenya (CIC) imesema kuwa, Waziri Mkuu wa nchi hiyo Raila Odinga na takriban mawaziri wote wako ofisini kinyume cha sheria.
Mwenyekiti wa CIC, Charles Nyachae amemuandikia barua Rais Mwai Kibaki akimtaka achukue hatua za haraka kuwaondoa ofisini maafisa hao wa serikali. Kwenye barua hiyo, Nyachae amenukuu kipengee cha katiba kinachowataka mawaziri kuachia ngazi punde baada ya kufanyika uchaguzi mkuu.
Mbali na Waziri Mkuu na mawaziri wengine, Nyachae pia amesema Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka anafaa kuondoka ofisini. Ingawa mwenyekiti huyo wa CIC amekiri kwamba serikali huenda ikashindwa kutekeleza majukumu mengi endapo mawaziri hao watalazimishwa kwenda nyumbani, lakini amesisitiza kuwa katiba ni lazime iheshimiwe na kutekelezwa kikamilifu.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO