Waasi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wameripotiwa kutwaa kasri la rais katikati ya mji mkuu Bangui. Hii ni baada ya mapigano makali kuzuka karibu na kasri hilo mapema leo. Duru za serikali zinasema kuwa Rais Francois Bozize amelazimika kukimbilia nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Mshauri wa rais ambaye hajataka kutajwa jina lake amesema Bozize leo amevuka mto Oubangi na kuingia Congo. Wapiganaji wa muungano wa waasi SELEKA waliingia mjini Bangui jana Jumamosi wakiapa kumwondoa madarakani Rais Bozize. Waasi wa SELEKA wamepuuza wito wa kufanya mazungumzo ya kuepusha umwagaji damu, baada ya kuvunjika kwa muafaka wa amani uliodumu miezi miwili katika nchi hiyo isiyo isiokuwa na utulivu na maskini kabisa.Kanali Djiuma Narkoyo, ambaye ni mmoja wa makamanda wa jeshi la SELEKA amewataka wanajeshi wa serikali kuweka chini silaha, kwa sababu leo ndio siku ya maamuzi.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO