Waziri wa Mambo ya Nchi za Kigeni wa Marekani John Kerry leo amefanya ziara ya ghafla mjini Baghdad, kuishinikiza Iraq kusaidia katika mgogoro unaoendelea nchini Syria, wakati kukiwa na madai ya kufifia kwa ushawishi wa Marekani ikiwa ni mwaka mmoja baada ya wanajeshi wa Marekani kuondoka nchini humo. Ziara hiyo ya kwanza nchini Iraq baada ya kupewa wadhifa huo, pia inaangazia hofu ya Marekani kwa vurugu zilizodumu miezi kadhaa katika mikoa ya nchi hiyo inayokaliwa na Wasunni wengi, zitanatowa nafasi zaidi kwa makundi ya wanamgambo ikiwa ni pamoja na al-Qaeda kuendesha harakati zao. Kerry atakutana na Waziri Mkuu Nuri al-Maliki na Spika wa bunge Osama al-Nujaifi na kuwashinikiza maafisa wa Iraq kushirikiana katika juhudi za kuutenga utawala wa rais wa Syria anayekabiliwa na shinikizo Bashar al-Assad. Marekani inaishtumu Iraq hasa kwa kunyamaza kimya wakati Iran ikituma vifaa vya kijeshi nchini Syria kupitia anga ya Iraq, safari ambazo serikali ya Tehran inasisitiza ni za kusafirisha misaada ya kibibaadamu pekee.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO