Rais Hamid Karzai wa Afghanistan amesema kuondoka majeshi ya kigeni nchini
mwake kutapelekea kuimarika hali ya usalama na amani.
Rais Karzai amesema wanajeshi wa kigeni ndio chanzo cha kudorora hali ya
usalama kutokana na jinsi wanavyoamiliana kikatili na wananchi wa Afghanistan.
Amefafanua kwamba, kutokana na wenyeji kuwachukia wavamizi wa kigeni, makundi ya
wanamgambo yamezidi kupata nguvu na uungaji mkono na hivyo kudhoofosha hali ya
usalama. Hamid Karzai amerudi kutoka Marekani ambako Rais Barack Obama amemshinikiza
akubali majeshi 9000 wa Marekani kubakia Afghanistan baada ya mwaka ujao wa 2014
ambapo majeshi yote ya kigeni yanapaswa kuondoka. Obama pia ametaka majeshi hayo
yapewe kinga ya kisheria ili mwanajeshi yeyote wa Marekani asiweze kushtakiwa
kwa makosa yoyote katika ardhi ya Afghanistan.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO