Tuesday, March 12, 2013

RAIS WA IRAN MATATANI BAADA YA KUMKUMBATIA MAMA WA CHAVEZ KATIKA MSIBA


Viongozi wakuu wa kidini nchini Iran wamemkosoa rais wa nchi hiyo Mahmoud Ahmadinejad kwa kumfariji mama wa rais Hugo Chavez wa Vnezuela kwa kumkumbatia,kitendo ambacho kinaangaliwa kama ni makosa kwa mujibu wa sheria kali za kidini nchini Iran.
Hatua hiyo ya viongozi wa kidini inatokana na kuchapishwa kwa picha hizo zinazomuonyesha rais Ahmedinejad akimkumbatia mama wa Chavez katika maziko ya kiongozi huyo wa Venezuela wiki iliyopita.Magazeti ya Iran yaliyotoka hii leo yamechapisha kauli hizo za viongozi mbali mbali wakuu wa kidini kutoka kituo kikuu cha kidini cha QOM ambao wamesema  kitendo hicho cha rais hakikubaliki na kinakwenda kinyume na sheria za kidini na taifa kwa jumla.Sheria za Iran ambazo zinatokana na misingi ya kidini zinamzuia mwanamme  kumkumbatia mwanamke ambaye sio wa familia yake.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO