Benki ya Dunia imeishutumu Israel juu ya mfumo wake wa kuweka vituo vya ukaguzi katika maeneo ya wapalestina na ikisema kwamba mfumo huo unachelewesha shughuli ya kutolewa kwa mamilioni ya dola ya fedha za malipo ya kodi ya mapato na kuzuia usafirishaji wa bidhaa kutoka Gaza,hatua ambayo imesababisha uharibifu wa muda mrefu wa uchumi wa Palestina.Benki hiyo ya dunia imetoa ripoti yake hiyo hii leo ambayo pia inasema kuzorota kwa miundo mbinu ya maji na usafiri ni matatizo makubwa hasa katika Gaza.Maafisa wa Israel wanasema hatua hizo zinachukuliwa kutokana na hali ya wasiwasi wa kiusalama.Aidha ripoti hiyo ya benki ya dunia imetaja kwamba matatizo ya wapalestina yanaongezeka kutokana na kukosa msaada wa wafadhili hatua inayoifanya mamlaka hiyo ya wapalestina kukopa kiwango kidogo cha fedha kisichotosheleza kutoka mabenki ya ndani.Uchumi wa Palestina umezorota ndani ya kipindi cha takriban miaka 20 huku biashara ikipungua kutoka asilimia 10 ya kiuchumi katika mwaka 1994 na kufikia asilimia 7 katika wakati huu ikiwa ni kiwango kidogo kabisa duniani.Ripoti hiyo imetolewa kabla ya mkutano wa wafadhili mjini Brussels uliopangiwa kufanyika tarehe 19.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO