Friday, March 22, 2013

SARKOZY KUCHUNGUZWA KESI YA UCHAGUZI

Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy anachunguzwa kutokana na kesi ya huko nyuma kuhusiana na kuchukua kinyemela fedha kwa ajili ya kampeni zake za uchaguzi kutoka kwa mwanamke tajiri zaidi wa nchi hiyo. Sarkozy anatuhumiwa kupokea maelfu ya Euro kutoka kwa mwanamke huyo tajiri Liliane Bettencourt mrithi wa kampuni kubwa ya vipodozi ya L'Oreal ambaye sasa ana miaka 90. Sarkozy ambaye hivi karibuni alisema kuwa atarejea tena kwenye ulingo wa siasa, amekana kutumia vibaya utajiri wa bibi huyo katika kampeni zake za uchaguzi. Iwapo atapatikana na hatia kiongozi huyo wa zamani Ufaransa atakabiliwa na kifungo cha miaka mitatu jela na faini kubwa, na huenda taswira yake ya kisiasa ikaharibika mno.
Bi. Bettencourt ambaye tangu 2006 anasumbuliwa na ugonjwa wa usahaulifu, ni mwanamke tajiri zaidi Ufaransa na Sarkozy anatuhumiwa kuchukua kinyume cha sheria kwa mwanamke huyo Euro 120,600 kwa ajili ya kampeni zake za urais.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO