Balozi wa Algeria nchini Libya amesema kuwa, watoto watatu wa Kanali Muammar Gaddafi pamoja na mjane wa dikteta huyo wa Libya aliyeuawa wameondoka nchini Algeria. Taarifa zinaeleza kuwa, Aisha na Hanibbal Gaddafi ambao wanatafutwa na polisi ya kimataifa ya Interpol kwa ombi la serikali ya Tripoli, pamoja na Muhamed Gaddafi na mjane wa dikteta huyo wa Libya Safia, wameondoka muda mrefu Algeria lakini haikuelezwa wameelekea wapi. Habari hizo za kutoweka familia ya Gaddafi huko Algeria sasa zimesambaa katika vyombo vya habari vya nchi za Kiarabu ingawa hawajulikani walipo. Familia ya dikteta wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi ilikuwa ikijulikana kwa maisha yake ya kifahari, huku baadhi ya wanafamilia hao wakiwa wawekezaji wakuu katika sekta za uchumi kama usafiri na mawasiliano.
Maafisa wa Libya bado hawajatoa matamshi yoyote kuhusiana na habari hiyo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO