Serikali ya Somalia imefikia makubaliano na kundi la wanamgambo wa Ahlu Sunnat Waljama’a ya kuingizwa wanamgambo hao kwenye jeshi la serikali ya nchi hiyo. Radio Mogadishu imetangaza leo kuwa, makubaliano hayo yamefanyika wakati huu ambapo Waziri Mkuu wa Somalia Abdi Farah Shirdon anafanya ziara ya kikazi katika mikoa ya kati ya nchini hiyo.
Kundi la wanamgambo wa Ahlu Sunnat Waljama’a limekuwa likidhibiti mikoa ya katikati mwa nchi hiyo. Miaka mitatu iliyopita, wanamgambo wa kundi hilo waliungana na jeshi la serikali katika mapambano dhidi ya wapiganaji wa kundi la al Shabab. Makubaliano kati ya serikali ya Somalia na kundi la Ahlu Sunnat Waljama'a ni hatua muhimu itakayozidisha nguvu na uwezo serikali kuu ya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO