Thursday, March 07, 2013

WASIWASI WAZIDI KUONGEZEKA KENYA

Nchini Kenya wasiwasi unazidi kuongezeka wakati  shughuli ya kuhesabu kura za uchaguzi mkuu na urais  ikiendelea kwa kasi ndogo kufuatia matatizo ya kimitambo katika vyombo vya elekroniki vinavyotumika katika shughuli hiyo. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa hivi punde na tume ya uchaguzi nchini humo IEBC matokeo yote yaliyowasilishwa katika kituo kikuu cha kupokea matokeo cha Bomas yamelazimika kuanza kuhesabiwa upya.Hata hivyo matokea ya mwanzo yanaonyesha kwamba Naibu waziri mkuu Uhuru Kenyatta anayekabiliwa na kesi katika mahakama ya ICC anaongoza katika kinyang'anyiro cha urais.Hata hivyo huenda akashindwa kupata ushindi wa moja kwa moja katika duru ya mwanzo.Kwa mujibu wa taarifa za shirika la habari la dpa wapiga kura wanazidi kuingiwa na wasiwasi juu ya kucheleweshwa kwa shughuli za kutangaza matokeo.Baadhi ya wanachi walionukuliwa na shirika la habari la dpa wanasema hali inayoshuhudiwa katika mtaa wa kibera ni ya wasiwasi mkubwa na wengi wameanza kupoteza subira.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO