Wizara ya Ulinzi ya Tunisia imekanusha taarifa kwamba ndege moja ya Libya isiyo na rubani imeanguka katika ardhi ya nchi hiyo. Mukhtar bin Nasr msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Tunisia amesea habari zilizotangazwa kuhusu kuanguka ndege ya Libya isiyo na rubani katika ardhi ya Tunisia ni za uwongo na zisizo na msingi wowote. Baadhi ya vyombo vya habari nchini Tunisia vimeripoti kuwa ndege ya Libya isiyo na rubani Jumatano iliyopita ilianguka katika eneo linaloungana na kitongoji cha Bin Qadran huko kusini mwa Tunisia karibu na mpaka wa Libya. Vyombo hivyo vya habari viliripoti kuwa, baadaye ilifahamika kuwa ndege hiyo isiyo na rubani mali ya Libya ilitengenezwa nchini Marekani baada ya vikosi vya jeshi la Tunisia kuwasili mahali ndege hiyo ilipoanguka.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO