Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amewasili nchini Italia leo kwa ajili ya kuhudhuria kutawazwa kwa Papa Francis na maafisa wamejaribu kupuuzia ukiukaji wa kiutaalamu wa marufuku ya kusafiri katika mataifa ya Umoja wa Ulaya dhidi ya kiongozi huyo wa siku nyingi barani Afrika.
Mugabe, ambaye amepigwa marufuku kuingia katika mataifa ya Ulaya tangu mwaka 2002 kwa sababu ya madai ya udanganyifu katika kura na ukiukaji wa haki za binadamu nchini Zimbabwe, alichukuliwa moja kwa moja kutoka katika ndege iliyomleta mjini Rome kwa gari, pamoja na mkewe, Grace na walinzi wake.
Licha ya kuwa uwanja huo wa ndege uko katika ardhi ya Italia, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 89 alilakiwa na padri, ambaye alimwambia: "Kwa niaba ya Papa Francis, karibu Vatican, karibu mahali patakatifu". Baadaye alipelekwa katika hoteli katika eneo maarufu la Via Veneto. Kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Francis, anatawazwa rasmi kesho Jumanne.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO