Saturday, March 16, 2013

UN YALAANI MASHAMBULIZI YA DRONE NCHINI PAKISTAN

Umoja wa Mataifa umelaani mashambulizi ya ndege za Marekani zisizotumia rubani nchini Pakistan, ukisema kuwa mashambulizi hayo hayajaridhiwa na serikali ya Pakistan, na hivyo yanakiuka sheria za kimataifa. Mwandishi wa ripoti wa Umoja wa Mataifa kuhusu mapambano dhidi ya ugaidi na haki za binaadamu Ben Emmerson, ambaye alikuwa nchini Pakistan kwa siku tatu kutathmini hali hiyo na kuzungumza na maafisa wa serikali ya nchi hiyo, amesema serikali ya Pakistan hairidhii matumizi ya ndege hizo ndani ya mipaka yake, na inachukulia vitendo vya Marekani kama ukiukaji wa uhuru wake. Maafisa wa serikali ya Pakistan walimuambia Emmerson, kuwa mashambulizi ya ndege hizo yana madhara kwa sababu yanacochea siasa kali miongoni mwa raia, na yanakiuka sheria za kimataifa, na kutaka matumizi ya ndege hizo kusitishwa mara moja.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO