Wednesday, March 13, 2013
VENEZUELA KUCHUNGUZA CANCER ILIYOMUUA CHAVEZ
Serikali ya Venezuela imesema kuwa itaanzisha uchunguzi rasmi ili kuchunguza madai kuwa ugonjwa wa saratani aliokuwa nao Hugo Chavez Rais wa nchi hiyo aliyeaga dunia ulisababishwa na maadui wa kigeni. Jumanne ya jana, Nicolas Maduro Kaimu Rais wa Venezuela aliahidi kuanzisha uchunguzi ili kuchunguza madai yaliyotolewa na watu wengi akiwemo Chavez mwenyewe kwamba maradhi yaliyosababisha kifo chake yalitokana na sumu aliyopewa. Maduro amesema serikali ya Caracas itawaalika wanasayansi wa nchi za nje kushirikiana na kamati ya nchi hiyo ili kuchunguza tuhuma hizo. Rais Hugo Chavez wa Venezuela alifariki dunia tarehe tano mwezi huu baada ya kuuugua saratani kwa muda wa miaka miwili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO