Shirika la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa Human Rights Watch, limewatuhumu askari wa Mali kwa kutenda vitendo vya kikatili katika vita vinavyoendelea hivi sasa nchini humo. Ripoti hiyo iliyotolewa mapema leo, imelaani vikali vitendo vya ukatili vinavyofanywa na askari wa nchi hiyo dhidi ya watu wa makabila maalumu nchini Mali. Shirika hilo la kutetea haki za binaadamu limetangaza kuwa, vitendo hivyo vilianza tangu yalipoanza mashambulizi ya askari wa Ufaransa nchini Mali na imeitaka serikali ya Bamako kuanzisha uchunguzi wa kina kuhusiana na jinai hizo. Matokeo ya uchunguzi wa shirika hilo ulioanza kazi zake tarehe 18 Februari mwaka huu nchini Mali, unaonyesha kwamba, uingiliaji wa kijeshi wa askari wa Ufaransa nchini humo, uliambatana na kushadidi kwa vitendo vya ukatili na hali ya mchafukoge vilivyofungua mlango kwa askari wa Mali kutenda vitendo vya ulipizaji kisasi na jinai nyinginezo dhidi ya waasi wa serikali ya Bamako. Kabla ya hapo Harakati ya Ukombozi ya Kitaifa ya Azawad nchini Mali, iliitaka Mahakama ya Jinai ya Kimataifa ICC kuanza uchunguzi wa makosa ya jinai yalizotendwa na askari wa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO