Marekani imeionya Iran hii leo kwamba itakabiliwa na hatari ya kutengwa zaidi na Jumuiya ya Kimataifa ikiwa itashindwa kushughulikia wasiwasi wa Umoja wa Mataifa juu ya mpango wake wa Kinuklia ambao nchi za Magharibi unashuku unanuiwa kutumika kwa malengo ya kijeshi.Umoja wa Ulaya pia umetumia nafasi ya mkutano wa bodi ya shirika la atomiki la IAEA kuishinikiza jamhuri ya kiislamu ya Iran kukomesha hatua ya kuwatatiza wachunguzi wa shirika hilo la IAEA wanaoendesha shughuli zao za utafiti juu ya mpango huo wa Iran.Iran hata hivyo imekanusha tuhuma hizo.Marekani pamoja na washirika wake katika nchi za Magharibi wametoa ishara kwamba wamepania kuilazimisha Iran kuwaruhusu waangalizi wake kuingia katika maeneo yake ya shughuli za Kinuklia pamoja na kukaguliwa stakabadhi zake licha ya kuweko mazungumzo marefu kati ya taifa hilo la Kiislamu na nchi zenye nguvu wiki iliyopita.Hata hivyo mjumbe wa Iran katika shirika la IAEA mjini Vienna amesema tuhuma dhidi ya nchi yake hazina msingi na kwamba shirika hilo ndilo la kulaumiwa na sio Iran kwa kushindwa hadi sasa kufufua uchunguzi uliokwama.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO