Watu wenye silaha waliofunika nyuso zao wamewateka nyara watalii wawili, mmoja kutoka Israel na mwanamke kutoka Ulaya katika rasi ya Sinai nchini Misri. Watalii hao walikuwa wakitalii kwa gari kati ya eneo la Taba karibu na mpaka wa Israel, na Dahab, ambalo ni eneo maarufu la mapumziko kusini, walipotekwa na mabeduini waliokuwa katika gari dogo la kubebea mizigo. Mashirika ya usalama ya Misri yanawasiliana na watekaji nyara hao kujaribu kuwashawishi waachie huru mateka hao. Watekaji nyara wa Kibeduini wamekuwa wakiwakamata mateka watalii huko nyuma kushinikiza kuachiwa kwa wenzao walioko jela. Mapema mwezi huu, mkuu wa kampuni ya mafuta ya Marekani ya ExxonMobil pamoja na mke wake walitekwa nyara.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO