Julia Gillard Waziri Mkuu wa Australia amewaomba radhi wananchi wa nchi hiyo kutokana na serikali ya nchi hiyo kutekeleza mpango wa kuwapora watoto kwa nguvu kutoka kwa mama zao. Bi Julia Gillard amesema kuwa, serikali ya nchi hiyo ilifuata kibubusa mpango ulioanzishwa na Kanisa Katoliki wakati ule. Akizungumza mbele ya wahanga 800 wa tukio hilo mbele ya bunge la nchi hiyo, Gillard amesema kuwa, ameamua kuomba radhi kutokana na kitendo hicho kisicho cha kibinadamu kilichofanywa na viongozi waliomtangulia miaka kadhaa iliyopita. Utafiti uliofanywa kuhusiana na kadhia hiyo kuanzia mwaka 1951 hadi 1975 unaonyesha kuwa, karibu watoto laki mbili na elfu ishirini na tano walitenganishwa na mama zao kwa madai kuwa waliwazaa watoto hao bila ya kufunga ndoa. Watoto hao walichukuliwa na serikali na kisha kukabidhiwa kwa watu wengine ili waweze kuwalea vizuri. Serikali ya Australia ilitekeleza mpango huo kwa kisingizio kwamba watoto hao watapata mazingira na malezi mazuri. Waziri Mkuu wa Australia amesisitiza kuwa, kitendo hicho kilikuwa si cha kimaadili na kiungwana na hali kadhalika kinakinzana na sheria.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO