Ofisi ya Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel imethibitisha kwamba utawala huo umeanzisha tena uhusiano wake na serikali ya Uturuki. Uhusiano wa Uturuki na utawala wa Israel uliingia dosari na kuvunjika, baada ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel kushambulia msafara wa meli zilizobeba misaada ya kibinadamu kwa Wapalestina wa Ukanda wa Gaza mwaka 2010 na kusababisha wanaharakati tisa wa Uturuki kuuawa. Taarifa zinasema kuwa, uhusiano huo umerejeshwa tena baada ya Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa Israel kuiomba radhi rasmi serikali ya Uturuki kuhusiana na tukio hilo. Taarifa zinasema kuwa, pande hizo mbili zitarejesha uhusiano wao wa awali ikiwa ni pamoja na kufunguliwa tena balozi, na kuondosha hatua za kisheria zilizowekwa na Uturuki dhidi ya wanajeshi wa Israel. Imeelezwa kuwa, miaka ya hivi karibuni, Uturuki ilitangaza kukata uhusiano wake na Israel ili kupata uungaji mkono kutoka nchi za Kiarabu. Mara baada ya kuanza machafuko nchini Syria, Uturuki ilikuwa mstari wa mbele kuyaunga mkono makundi ya kigaidi nchini Syria kwa kuyapatia kambi za kijeshi katika maeneo ya mpakani na kuwapelekea magaidi misaada ya kifedha, kilojistiki ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya kijeshi na utumiaji silaha za kisasa kwa magaidi hao. Syria inakabiliwa na mashinikizo makubwa ya nchi za Magharibi na hasa Marekani, Uingereza na Ufaransa pamoja na nchi nyingine za Kiarabu kama vile Saudi Arabia, Qatar na hata Uturuki kutokana na misimamo yake ya kuunga mkono muqawama na mapambano ya Kiislamu ya wananchi wa Palestina dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO