Seriakli ya Iraq imekifungia kituo cha televisheni cha kimataifa cha Aljazeera na vituo vingine tisa vya nchini humo siku ya Jumapili, baada ya kivituhumu kwa kuchochea vurugu za kidini.
Hatua hii imemulika wasiwasi unaozidi wa serikali inayoongozwa na washia, juu ya hali ya usalama inayozidi kudorora, wakati wa machafuko ya waumini wa kisunni na makabiliano yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 180 katika muda wa chini ya wiki moja. Kusimamishwa kwa vituo hivyo ambako utekelezaji wake ulianza mara moja kunaonekana kuvilenga hasa vituo vya kisunii vinavyojulikana kwa kuikosoa serikali ya waziri mkuu Nouri al-Malik. Pamoja na kituo cha Aljazeera, uamuzi huo uliviathiri vituo nane vya kisunni na kimoja cha kishia. hatua hii ya serikali imekuja huku utawala mjini Baghdad ukijaribu kukabiliana na ongezeko la machafuko nchini humo, yaliyoripuka siku chache zilizopita, baada ya vikosi vya usalama kuanzisha operesheni ya ukandamizaji dhidi ya kambi ya waandamanaji wa kisunni katika mji wa kati wa Hawija, na kuua watu 23, wakiwemo wanajeshi watatu.
Tangu wakati huo, zaidi ya watu 180 wameuawa katika mapigano na vikosi vya usalama na mashambulizi mengine. Wimbi la hivi karibuni la vurugu linafuatia miezi minne ya maandamano ya amani ya waislamu wa madhehebu ya sunni, dhidi ya serikali ya waziri mkuu Nouri al-Maliki. Watazamaji nchini Iraq watanedelea kutizama vituo hiyvo, lakini tangazo la kusitishwa kwake lililotolewa na tume ya mawasiliano na vyombo vya habari linasema kama vituo hivyo kumi vitajaribu kuendesha shughuli zake katika ardhi ya Iraq, vitakabiliwa na hatua za kisheria kutoka kwa vyombo vya usalama. Kimsingi amri hiyo inawazuia wanahabari kutoka vituo hivyo kufanya kazi zao nchini Iraq.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO