Thursday, April 11, 2013

CHINA YASISITIZA HAKI YA IRAN KUWA NA NYUKLIA

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Hong Lei amesisitiza kuhusu haki ya Iran ya kunufaika na nishati ya nyuklia kwa mujibu wa Mkataba wa Kuzuia Uundaji na Usambazaji Silaha za Nyuklia NPT na mikataba husika ya kimataifa.
Hong Lei ametoa wito kwa Iran na kundi la 5+1 kuandaa mazingira ya kutatuliwa kwa amani mgogoro ulioibuliwa na nchi za Magharibi kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.
Nchi za 5+1 zinajumuisha Uchina, Russia, Ufaransa, Uingereza, Marekani na Ujerumani.
Mwanadiplomasia huyo wa China amesema Beijing iko tayari kushirikiana na pande husika ili kutatua hitilafu zilizopo.
Mazungumzo ya Iran na kundi la 5+1 yalimalizika Almaty, Kazakhstan Aprili 6. Baada ya kikao hicho Saeed Jalili, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran alisisitiza kwa mara nyengine tena juu ya haki ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kurutubisha urani.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO