Thursday, April 11, 2013

WAZIRI MKUU WA PALESTINA ATAKA KUJIUZULU

Waziri Mkuu wa Mamlaka ya ndani ya Palestina, Salam Fayyad, anatarajiwa kujiuzulu hivi leo kwa sababu ya ongezeko la mzozo baina yake na Rais Mahmoud Abbas kuhusiana na kiwango cha madaraka yake. Abbas hajamjibu Fayyad, ambaye anaungwa mkono na nchi za magharibi, na hasa Marekani. Haijabainika wazi kama Abbas, anayetarajiwa kuwasili katika Ukingo wa Magharibi leo kutoka ziara ya Qatar, atakubali ombi la kujiuzulu Fayyad katika wakati ambapo Marekani inajaribu kuyafufua mazungumzo ya amani baina ya Israel na Palestina. Kama sehemu ya juhudi hizo, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani, John Kerry, anataraji kupata idhini ya Israel kuhusu miradi ya kiuchumi ya Palestina katika Ukingo wa Magharibi. Fayyad, ambaye ni mwanauchumi maarufu, anaonekana kuwa mtu muhimu anayeweza kusimamia miradi ya aina hiyo. Uhusiano kati ya Fayyad na Abbas umekuwa wenye hofu kwa muda sasa, na Waziri huyo mkuu tayari alimwambia Abbas mwishoni mwa mwaka jana kuwa alitaka kujiuzulu.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO