Mahakama moja nchini Pakistan leo imeamuru kukamatwa kiongozi wa zamani wa kijeshi Pervez Musharraf kuhusiana na uamuzi wake wenye utata wa kuwafuta kazi majaji wakati alipotangaza sheria ya hali ya hatari mnamo mwaka wa 2007. Haijabainika wazi ikiwa jenerali huyo mstaafu atakamatwa. Musharraf aliondoka katika mahakama ya Islamabad, bila kuzuiwa na mafisa wa usalama waliokuwa wamejaa nje ya mahakama, na kuondoka ndani ya gari lake akisindikizwa na walinzi wake. Msemaji wa chama chake amesema kiongozi huyo atawasilisha kesi katika Mahakama ya Juu kupinga amri ya kukamatwa kwake. Musharraf anakabiliwa na mashitaka ya kupanga njama ya mauwaji ya kiongozi wa upinzani Benazir Bhutto mwaka wa 2007, na kuhusiana na kifo cha kiongozi wa waasi kabila la Baluch wakati wa operesheni ya kijeshi mwaka wa 2006. Rais huyo wa zamani alirudi nyumbani tarehe 24 mwezi uliopita,baada ya kuishi uhamishoni kwa miaka minne nchini Dubai na Uingereza, na kuahidi kugombea katika uchaguzi mkuu.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO