Saturday, April 27, 2013

MSAMAHA KWA WAASI WA SUDAN

Makundi kadhaa ya waasi yanayoendesha harakati zao katika maeneo yenye utajiri wa mafuta kaskazini ya Sudan Kusini yamekubali pendekezo la msmaha wa serikali ili nao wasitishe uasi. Makundi ya waasi ya South Sudan Liberation Army, South Sudan Democratic Army na South Sudan Defense Forces, yote yamelikubali pendekezo hilo la msamaha la Rais Salva Kiir. Gazeti la Tribune limesema leo kuwa kundi la South Sudan Democratic Liberation Army, likiongozwa na David Yau Yau, ni kundi pekee lililougomea msamaha huo. Yau Yau anaongoza wapiganaji wa kabila la Murle, ambao wamekuwa wakipigana na serikali katika jimbo la Jonglei ambalo limekumbwa na mapigano makali ya kikabila katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Kwa ujumla, serikali ilitangaza msamaha kwa makamanda sita wakuu wa waasi na manaibu wao kwa kufanya uasi Makundi yaliyokubali msamaha huo yatakutana karibuni na Rais Kiir mjini Juba ili kukamilisha mpango huo na kuafikiana namna ya kuwajumuisha wapiganaji wao katika jeshi la kitaifa.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO