Mufti wa Libya ameitaka serikali ya nchi hiyo kupiga marufuku vinywaji vyote vyenye kileo na madawa ya kuvya. Sadiq Al-Ghiryani amewataka viongozi wa serikali ya Tripoli kukabiliana na uuzaji wa vileo hadharani na madawa ya kulevya nchi humo. Al-Ghiryani amesisitiza juu ya ulazima wa serikali na viongozi wa Libya kupambana na vitendo vyote vinavyokwenda kinyume na mafundisho ya Kiislamu na kuwataka Walibya wote wapambane na vitendo vilivyokinyume na mafundisho ya dini Tukufu ya Kiislamu, ukiwemo unywaji pombe na madawa ya kulevya.
Vilevile Mufti wa Libya amesema katika kuungana na familia dhidi ya vitendo viovu, serikali lazima ifunge mitandao yote ya internet ambayo inakinzana na maadili mema.
Kwa mujibu wa sheria za Libya, ni marufuku kutumia vinywaji vyenye kileo na dawa za kulevya na adhabu kali inatolewa kwa makosa hayo. Hata hivyo vileo na dawa za kulevya zimeongezeka kwa kiwango kikubwa nchini Libya kutokana na ukosefu wa usalama.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO