Sunday, April 14, 2013

VENEZUELA YACHAGUA RAIS MPYA LEO


Uchaguzi wa rais Venezuela unafanyika leo Jumapili huku serikali ya nchi hiyo ikisema imevunja njama za mamuluki wa kigeni waliopanga kuvuruga uchaguzi huo wa kumtafuta mrithi wa marehemu Hugo Chavez.
Makamu wa Rais wa  Venezuela Jorge Arreaza amesema vikosi vya usalama vimewatia nguvuni mamuliki kutoka Colombia ambao walikuwa wanapanga kuibua ghasia katika uchaguzi wa leo. Henrique Capriles, kiongozi wa upinzani nchini humo anayeungwa mkono na Marekani, anachuana na  Nicolas Maduro, aliyekuwa Makamu wa Rais wa hayati Hugo Chavez, na ambaye kwa sasa ni rais wa mpito wa nchi hiyo.
Nicolas Maduro amesisitiza kuwa ataendelea kufuata siasa zile zile za kimapinduzi za rais aliyemtangulia hayati Hugo Chavez. Maduro mwenye umri wa miaka 50, alianza harakati zake za kisiasa wakati akiwa kijana mdogo na kwa uungaji mkono wa harakati ya kimapinduzi inayofahamika kwa jina la Bolivari huku akiwa dereva wa basi na kuwakilisha wafanyakazi wa jumuiya ya usafirishaji ya mjini Caracas. Kiongozi huyo ameonya kuwa, huduma zote za kijamii zinazotolewa kwa wasiojiweza Venezuela zitasimama ikiwa Henrique Capriles atachaguliwa kuiongoza nchi hiyo ya America ya Latini. Uchunguzi wa maoni unaonyesha kuwa Maduro atamshinda Capriles katika uchaguzi huo wa leo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO