Mataifa ya Magharibi yamesema yana ushahidi wa kutosha kuwa silaha za kemikali zilitumika angalau mara moja katika vita vya Syria. Serikali ya Rais Bashar al Assad imeutaka Umoja wa Mataifa kuchunguza madai yake dhidi ya waasi, lakini imekataa kuruhusu wataalamu wa kimataifa kuingia nchini humo kwa sababu ya kile ilichosema ni hujuma dhidi ya jeshi la Assad. Balozi mmoja kutoka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa amesema kuna ushahidi wa kuaminika ambao umetumwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja huo, Ban Ki Moon, kudhihirisha kuwa majeshi ya Assad yalitumia silaha hizo za kemikali. Uingereza na Ufaransa zimewasilisha taarifa kwa Umoja wa Mataifa kuhusu madai hayo ya jeshi kutumia silaha za kemikali katika mji wa Homs tarehe 23 Disemba mwaka jana na katika eneo la Ataybah karibu na mji mkuu, Damascus, mwezi uliopita. Kufikia sasa zaidi ya watu elfu sabini wameshauwawa katika vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO