Friday, April 12, 2013

UFARANSA YAIDHINISHA LAANA YA KUOANA JINSIA MOJA

Bunge la Senate nchini Ufaransa limepitisha mswada wa kuhalalisha ndoa za watu wa jinsia moja na hivyo basi kutoa fursa ya kuwa sheria baada ya maandamano ya maelfu ya waandamanji wa pande zote mbili wanaopinga na kuunga mkono ndoa za aina hiyo. Hatua hiyo ni muhimu nchini Ufaransa tangu sheria ya mwaka 1981 ya kuondoela mbali hukumu ya kunyongwa na ilikuwa mojawapo ya ahadi kuu katika kampeni za Rais Francois Hollande. Lakini inapingwa na chama cha kihafidhina katika taifa lililo na Wakatoliki wengi na Waislamu nchini humo. Mswada huo uliopitishwa kwa wingi wa kura katika bunge hilo unasubiri kuidhinishwa na kuanza kutekelezwa katikati ya mwaka huu. Ufaransa inaungana na mataifa mengine 11 yaliyohalalisha ndoa za wtu wa jinsia moja zikiwemo Ubelgiji, Ureno, Uholanzi, Uhispania, Sweden, Norway na Afrika ya Kusini.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO