Wednesday, April 10, 2013

WANANCHI WASHEREHEKEA KIFO CHA WAZIRI MKUU WA ZAMANI

Serikali ya Uingereza imetangaza kuwa, Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Margaret Thatcher atazikwa Jumatano ya wiki ijayo Aprili 17. Thatcher aliyefariki dunia siku ya Jumatatu atafanyiwa mazishi ya kiserikali yatakayoandamana na heshima kamili ya kijeshi. Habari zaidi zinasema kuwa Malkia wa Uingereza na mume wake watahudhuria marasimu hiyo. Huku hayo yakijiri, shangwe na nderemo zimeshuhudiwa katika maeneo mbalimbali punde baada ya kuenea habari ya kufariki dunia Waziri Mkuu huyo wa zamani. Huko Scotland mamia ya watu wamejitokeza kushangilia kifo cha Thatcher na wamewaambia wanahabari kuwa, kiongozi huyo wa zamani ni nembo ya dhulma na matatizo yanayowakabili kwa sasa. Hali hiyo pia imeshuhudiwa katika miji ya Brixton na Leeds. Thatcher ambaye ndiye mwanamke wa pekee kuwahi kushikilia wadhifa wa Waziri Mkuu nchini Uingereza, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO