Tuesday, April 23, 2013

WATUHUMIWA WA UBAKAJI WA MTOTO INDIA WAKAMATWA


Jeshi la polisi nchini India linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za ubakaji wa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitano tukio ambalo liliibua hisia kali na kusabababisha maandamano makubwa ya kupinga vitendo vya ubakaji katika mji wa New Delhi. Watuhumiwa hao wawili kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka ya utekaji na ubakaji wa mtoto huyo. Madaktari katika hospitali ya serikali ya New Delhi wamesema hali ya mtoto huyo kwa sasa inazidi kuimarika na wanaendelea kufanya jitihada kuhakikisha afya yake inakuwa njema.
Aidha waandamanaji wanataka Mkuu wa polisi wa New Delhi aondolewe katika ofisi yake kutokana na jeshi lake kushindwa kufanya kazi yake ipasavyo kwani limekuwa likipuuza madai mbalimbali yanayowasilishwa kwao. Waziri Mkuu wa India Manmohan Singh ametoa wito kwa kila mwananchi kushiriki kuwasaidia wanawake na watoto wa kike ambao wamekuwa wakiishi kwa hofu kutokana na vitendo vya ubakaji kuzidi kushika kasi katika nchi hiyo.

Vitendo vya ubakaji kwa wanawake na watoto vimekuwa vikiripotiwa kila uchao katika vyombo vya habari nchini India, miito mbalimbali imezidi kutolewa kwa serikali ya nchi hiyo kuhakikisha wahusika wa makosa hayo wanapewa adhabu kali hasa baada hisia zilizozuka mwishoni mwa mwaka jana baada ya tukio la kubakwa mpaka kufa kwa msichana mwenye umri wa miaka 23 aliyekuwa mwanafunzi wa udaktari. Tayari sheria ya nchi hiyo imefanyiwa marekebisho na kujuisha kipengele cha adhabu ya kifo katika makosa ya ubakaji.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO