Waziri Mkuu wa Syria, Wael al-Halqi amepongeza mafanikio ya jeshi la nchi hiyo katika vita dhidi ya waasi wanaoungwa mkono na Wamagharibi na kusisitiza kuwa serikali inakaribia kupata ushindi mkubwa. Waziri Mkuu huyo amesema kuuawa kamanda mkuu wa kundi la waasi la Jabhat an-Nusra huko Qusayr pamoja na kudhibitiwa miji kadhaa iliyokuwa imetekwa na waasi ni dalili nzuri zinazoashiria kwamba serikali itawashinda waasi. Hii ni katika hali ambayo, Rais Bashar Asad alitangaza siku ya Jumamosi iliyopita kwamba waasi kutoka zaidi ya nchi 29 wanapigana na serikali huko Syria. Rais Asad alisema wageni wanaopigana na serikali ndio wanaozidi kuharibu hali ya mambo. Jamii ya Kimataifa ikiongozwa na Russia, China na pia Marekani zimesisitiza kuwa mgogoro wa Syria unafaa kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO