Msemaji wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF), Gerry Rice amesema kuwa uchumi wa Misri unaendelea kuporomoka na amedokeza kuwa Cairo haitopata msaada wowote kutoka kwa shirika lake hadi pale itakapotoa ripoti mpya kuhusu hali halisi ya kiuchumi. Mazungumzo ya IMF na Misri kuhusu mkopo wa dola bilioni 4.8 yameshindwa kukamilika kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa kutokana na kile kinachotajwa kuwa ni woga wa Cairo wa kuchukua maamuzi magumu. Serikali ya Misri itatakiwa kupunguza matumizi, kuondoa ruzuku katika bidhaa nyingi hususan mafuta na gesi pamoja na kupunguza idadi ya wafanyakazi wa umma kabla ya kupokea mkopo huo. Weledi wa mambo wanaamini kuwa. Cairo haiko tayari kuchukua hatua hizo kwa hofu kwamba wananchi wataandamana na huenda wakaiangusha serikali ya Rais Mohammad Mursi.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO