Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema leo kuwa amejadiliana na waziri mkuu wa Uingereza David Cameron uwezekano na hatua za pamoja za kumaliza mzozo nchini Syria. cameron aliwasili leo katika mji wa Sochi, kusini mwa Urusi kwa majadiliano na rais Putin kuhusiana na hatua za kuchukuliwa kumaliza mzozo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.
Wakati huo huo Kamishna wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa Navy Pillay ameeleza wasi wasi wake kuhusu kupelekwa kwa majeshi ya Syria karibu na mji unaoshikiliwa na waasi wa Qusair magharibi ya nchi hiyo. Mji huo umezingirwa na majeshi ya Syria kwa wiki kadhaa sasa na waasi wamepoteza nguvu za kulidhibiti eneo hilo.
Pillay alisema mauaji ya halaiki ya wiki iliopita yanapaswa kutoa chachu kwa jumuiaya ya kimataifa itafute suluhisho la haraka la mzozo huo wa miezi 26 sasa nchini Syria.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO