Iran imewanyonga leo majasusi wawili waliohukumiwa kwa kupatikana na hatia ya kuifanyia kazi Israel, na Marekani. Mohammed Heydari alihukumiwa kwa kupokea malipo ili kutoa habari za kijasusi kuhusu masuala kadhaa ya usalama na siri za taifa katika mikutano mingi baina yake na shirika la ujasusi la Israel, Mossad. Naye Koroush Ahmadi alipatikana na hatia ya kutoa habari za kijasusi kuhusiana na masuala tofauti kwa Shirika la Ujasusi la Marekani - CIA. Taarifa hiyo ya waendesha mashitaka haikutoa maelezo zaidi. Iran inawashutumu mahasimu wake Israel na Marekani kwa kufanya kampeni mbaya ya hujuma dhidi ya mpango wake wa nyuklia na imetangaza kuwakamata katika miaka ya karibuni watu kadhaa wanaoshukiwa kuwa majasusi.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO