Sunday, May 19, 2013

RAIS ASAAD ASISITIZA KUTOJIUZULU

Rais wa Syria Bashar al-Assad, amesisitiza kuwa hawezi kuwachia madaraka kama  anavyotakiwa na nchi za magharibi, ikiwa ni pamoja na Marekani na upinzani nchini Syria. Akizungumza katika mahojiano ya nadra na gazeti moja la Argentina, Assad ameukaribisha mpango wa pamoja wa Marekani na Urusi wa kuandaa mkutano wa amani mjini Geneva, lakini ametupilia mbali uwezekano wa kufanya mazungumzo na makundi ya wanamgambo. Bomu la kutegwa ndani ya gari liliripuliwa jana katika vitongoji vya mji mkuu Damascus. Ripoti za kutatanisha zimeiweka idadi ya vifo kuwa kati ya watu watatu na wanane. Kundi la Kutetea Haki za Binadaamu la Syria limesema watu waliokuwa na bunduki wamemteka nyara babake Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Syria, Faisal Muqdad, ambaye ni kiongozi muhimu katika utawala wa Assad, katika mkoa wa Kusini wa Daraa, katika tukio la kulipiza kisasi ukamataji uliofanywa na serikali.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO