Majenerali wa Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel wameliomba baraza la mawaziri la utawala huo haramu litoe kibali cha kushadidisha ukandamizaji dhidi ya Wapalestina wa Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan. Gazeti la Kizayuni la Maariv limeandika kuwa majenerali wa jeshi la Israel wanasisitiza kuwa kuna ulazima wa kuchukua hatua kali zaidi za ukandamizaji ili kukomesha machafuko katika eneo la Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan. Maariv limemnukuu Jenerali Danny Yatom akisema kuwa baraza la mawaziri linapaswa kutoa kibali haraka kwa jeshi ili lichukue hatua kali zaidi za ukandamizaji dhidi ya Wapalestina na kuzuia kuenea machafuko na kuanza Intifadha ya Tatu. Yatom, ambaye ni mkuu wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Israel Mossad amesema jeshi la Israel haliwezi kubaki kuwa mtazamaji tu wa machafuko katika Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan bali linapaswa kutoa radiamali na kuwaua wapinzani. Jenerali huyo wa zamani wa jeshi la utawala haramu wa Israel amesisitiza juu ya ulazima wa kuwaua Wapalestina wa umri wowote ule na kubainisha kwamba bila ya kuhofu chochote vikosi vya jeshi la Israel vichukue hatua ya kumfyatulia risasi Mpalestina wa umri wowote ule atakayekuwa na jiwe mkononi mwake
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO