Askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamewateka nyara Wapalestina 25 waliokuwa wakiandamana huko mashariki mwa mji wa Quds. Maandamano hayo yalikuwa ya kumbukumbu ya kutimia mwaka wa 65 tangu ardhi za Palestina zianze kukaliwa kwa mabavu na Israel, siku inayojulikana kwa jina la “Naqba” yaani nakama. Askari katili wa utawala wa Kizayuni walitumia gesi za kutoa machozi, mabomu ya kupoozesha mwili na mabomba ya maji machafu ya sumu ili kuwatawanya waandamanaji hao wa Kipalestina na baadaye kuwateka nyara Wapalestina 25 na kuwapeleka kusikojulikana.
Katika upande mwingine wakimbizi wa Kipalestina wameshambuliwa na waasi wa Syria wanaofadhiliwa na nchi za kigeni katika kambi ya wakimbizi mjini Damascus. Tukio hilo limejiri kwenye kambi ya Yarmuk, mjini Damascus.
Wapalestina wa kambi hiyo wamelaani vikali kitendo hicho cha kigaidi cha waasi wa Syria wakisema kuwa waasi hao hawana hata hisia za kibinaadamu.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO