Thursday, May 16, 2013

WAFADHILI WAAHIDI KUISAIDIA MALI

Rais Francois Hollande wa Ufaransa amesema kuwa wafadhili wa kimataifa wameahidi kutoa msaada wa Euro milioni 3.25 kwa ajili ya kuijenga upya nchi ya Mali. Hollande amesema, msaada huo umeahidiwa kutolewa katika mkutano uliofanyika mjini Brussels Ubelgiji na kuhudhuriwa na wawakilishi 100 kutoka pande mbalimbali za dunia, kwa lengo la kujadili njia za kuisaidia nchi ya Mali kujinasua kwenye mgogoro iliotumbukia ndani yake. Rais wa serikali ya mpito ya Mali, Diancounda Traore naye pia amesifu mkutano huo na kusema kuwa ulikuwa wenye mafanikio kuliko walivyotegemea. Ufaransa ilianza mashambulizi ya kijeshi nchini Mali Januari 11 mwaka huu kwa kisingizio cha kupambana na waasi wa nchi hiyo, mashambulizi ambayo yameitumbukiza Mali kwenye mgogoro mkubwa wa kibinaadamu. Maelfu ya wananchi wa kaskazini mwa nchi hiyo wamekimbia makazi yao na hivi sasa wanaishi katika mazingira magumu kama wakimbizi.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO