Umoja wa Mataifa umemtangaza Jenerali Carlos Alberto dos Santos Cruz kuwa Kamanda wa Vikosi vya Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Jenerali Cruz raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 61alikuwa kamanda wa vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini Haiti kuanzia mwaka 2007 hadi 2009. Jenerali Cruz anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali Chander Prakash raia wa India ambaye amemaliza muda wake wa miaka miwili wa kuhudumu nchini Kongo. Imeelezwa kuwa, uteuzi wa kamanda huyo ulichelewa kidogo ili kutoa fursa kwa serikali ya Afrika Kusini kupendekeza afisa wa ngazi za juu wa jeshi atakayechukua jukumu hilo, lakini ilishindwa kumpata afisa wa jeshi mwenye uwezo wa kuzungumza kwa ufasaha lugha ya Kifaransa.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO