Tuesday, May 14, 2013

JESHI LA MALI LAELEKEA NGOME YA WAASI


Vikosi vya jeshi la Mali hii leo vimeelekea kwenye mji wa kaskazini mashariki wa Kidal ikiwa ni kabla ya muda uliopangwa na serikali wa kuukomboa kutoka katika mikono ya waasi wa Tuareg wanaotaka kujitenga.
Vikosi vya Ufaransa vilivyokuwa vikipambana na waasi kaskazini mwa Mali viliwaruhusu waasi wa MNLA kudhibiti mji wa Kidal katika miezi ya hivi karibuni, lakini serikali ya Mali inataka kuudhibiti mji huo kabla ya uchaguzi wa rais na Bunge unaotarajiwa kufanyika mwezi Julai. Waziri wa Ulinzi wa Yamoussa Camara alisema bungeni mwezi huu kwamba, swali kuhusiana na kudhibitiwa mji wa Kidal na waasi wa MNLA litajibiwa ifikapo Mei 15.
Waasi wa MNLA walikataa wito wa serikali ya Bamako wa kuweka chini silaha, wakisema kuwa watakabiliana na jitihada zozote za serikali za kudhibiti tena mji wa Kidal, lakini walisema mlango wa mazungumzo ya kisiasa na serikali upo wazi.
Katika upande mwingine Rais wa Chad ametangaza kuwa, askari wa nchi hiyo waliokuwa wakipigana nchini Mali na makundi ya waasi, wanaanza kurejea nchini kwao.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO