Frank Ribery mchezaji Muislamu wa klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani, ameapa kutoongea tena na mchezaji mwenzie wa timu hiyo Jerome Boateng baada ya kumwagia mwilini pombe, wakati wa wakishangilia ubingwa wa Bundesliga mwisho wa wiki iliyopita.
Mfaransa huyo ambaye ni mchamungu wa swala tano na ambaye jina lake la Kiislamu ni 'Bilal' alijaribu kumkimbia Boateng ili aepukane na kitendo cha ushangiliaji wa kumwagiana pombe wa wachezaji wenzie baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo, ambapo Bayern Munich walioshinda 3-0 dhidi ya Augsburg.
Lakini pamoja na kujaribu sana kukwepa kuguswa na pombe ambayo ni haramu kwa mujibu wa dini yake, Ribery hatimaye aliogeshwa na pombe hiyo mwili mzima na mchezaji mwenzake Boateng mwenye asili ya Kiafrika.
Ribery 'Bilal' alionyesha kukasirishwa mno na kitendo hicho, na kusisitiza kuwa: 'Sitoongea tena na Boateng, anajua mie ni Muislam. Nimechikizwa sana na kitendo chake.'
Mlinzi David Alaba na kiungo Anatoliy Tymoshchuk pia walijiunga na Boateng kumlowesha pombe Ribery, ambaye alionekana kutulia kwa wakati huo.
Golikipa Manuel Neuer kwa busara kabisa yeye alijiepusha na suala hilo na kuamua kuwamwagia baadhi ya mashabiki walioonekana kupendezewa na ushangiliaji huo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO