Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tunisia imelizuia kundi haramu la Mawahabbi linalojiita Ansar al Sharia kufanya mkutano wa kila mwaka katika mji wa Kairouan.
Katika taarifa, wizara hiyo imesema kundi hilo limeonyesha kuwa ‘haliheshimu taasisi za kiserikali’, ni ‘tishio kwa usalama wa umma’ na ‘linajihusisha na vitendo vya utumiaji mabavu.’
Sheikh Rashid al-Ghannushi kiongozi wa chama tawala cha Kiislamu cha Ennahdha ambacho kina misimamo ya wastani ameonya kuwa serikali haitaruhusu kufanyika kongamano hilo la kila mwaka la Mawahabbi. Ripoti zinasema watu 40 elfu walikuwa wamepanga kushiriki katika kongamano hilo. Kuna wasi wasi wa kutokea machafuko leo baada ya Mawahabbi kusema watakiuka amri ya serikali kupiga marufuku mkutano wao.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO