Makombora mawili yaliyorushwa kutoka Syria yameanguka katika eneo la mlima Hermon nchini Israel leo Jumatano tukio ambalo hata hivyo halijasababisha madhara yoyote msemaji wa jeshi amearifu. Msemaji huyo ameongeza kuwa milipuko miwili imesikika upande wa Israel kwenye mlima Hermon na kwamba wanaendelea na uchun guzi wa tukio hilo ambalo wanaamini ni matokeo ya hali ya mambo nchini Syria.
Eneo maarufu la Golan awali lililazimika kufungwa kuzuia wageni na kisha kufunguliwa tena baadaye na kwamba Israel imeviarifu vikosi vya umoja wa Mataifa UN katika eneo hilo kuhusu tukio hilo. Vilima vya Golan vimekuwa vikihofiwa tangu kuanza kwa mgogoro wa Syria zaidi ya miaka miwili iliyopita, wakati huo huo kumekuwa na milipuko midogo katika eneo hilo hadi sasa na makombora ya Syria yakirushwa katika vilima vya Golan na Israel kujibu mashambulizi.
Mvutano mkubwa umekuwepo baina ya Israel na Syria baada ya Israel kufanya shambulio la anga mjini Damascus mnamo Maei 3 na 5, na kuigadhabisha Syria ambayo ilisema kuwa itajibu mashambulizi ya Israel katika ngome yake kwa haraka.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO