Maelfu ya raia wa Bangladesh na Myanmar wameendelea kuhama katika maeneo ya pwani kufuatia hofu ya kimbunga cha Mahasen chenye kasi ya zaidi ya kilometa 100 kwa saa kinachotarajiwa kuikumba pwani ya nchi hizo mbili za barani Asia. Umoja wa Mataifa UN umesema huenda zaidi ya watu milioni nne nukta moja maisha yao yakawa hatarini kutokana na kimbunga hicho kinachotarajiwa siku ya Alhamisi.
Tayari Bangladesh imewahamisha raia wake zaidi ya laki saba wanaoishi katika maeneo hatarishi wakati Myanmar ikitangaza kuwahamisha raia wake zaidi ya laki moja na sitini katika eneo la pwani ya Kaskazini Mashariki. Bandari katika mji wa Chittagong wa Bangladesh imefungwa kutokana na mawimbi makali zaidi kutarajiwa kupiga katika pwani ya mji huo, inaelezwa kuwa tayari kimbunga hicho kimesababisha vifo vya watu zaidi ya sita nchini Sri-Lanka.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO