Wafanyakazi wa mwisho waliobakia wa Korea Kusini katika kiwanda cha pamoja ndani ya Korea kaskazini wamerejea nyumbani leo. Kurudi kwao kuanakamilisha hatua ya kuondoka kwa Korea kusini katika eneo hilo, kukiwa na hali ya wasiwasi mkubwa katika rasi ya Korea.
Msemaji wa serikali mjini Seoul alisema kulipatikana maelewano juu ya masuala ya malipo yaliosalia na Korea Kaskazini na hatimae Wakorea Kusini kukubaliwa kuvuka mpaka kurudi nyumbani. Kurejea nyumbani kwa wafanyakazi saba kutoka kiwanda cha Kaesong kulizuiliwa tangu Jumatatu, baada ya Korea Kaskazini kuadai malipo ya mishahara ya nyuma pamoja na kodi inayokadiriwa kufikia karibu dola milioni 80.
Korea Kusini iliamua kujiondoa katika eneo hilo la kiviwanda la pamoja wiki iliopita, baada ya Korea Kaskazini kukataa wito wa mazungumzo juu ya kufunguliwa tena kiwanda cha Kaesong. Shughuli zilisisimamishwa tarehe 19 mwezi uliopita, wakati Korea Kaskazini ilipowaondoa wafanyakazi wake 53,000, kwa sababu ya mazoezi ya kijeshi ya Marekani na Korea Kusini pamoja na mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO