Serikali ya Korea Kaskazini imesema iko tayari kufanya mazungumzo na Marekani ili kuondoa hali ya taharuki na wasiwasi katika Peninsula ya Korea. Pyongyang imesema iwapo Washington itaonyesha irada ya kufanya mazungumzo ya kweli basi viongozi wake wako tayari kwa mazungumzo. Korea Kaskazini imeitaka Marekani kuchagua tarehe na mahali pa kufanyika mazungumzo hayo. Washington haijasema lolote kuhusu pendekezo hilo lakini weledi wa mambo wanaamini kwamba Rais Obama huenda akakimbilia fursa hiyo kwani kadhia ya nyuklia ya Pyongyang ni miongoni mwa mambo yanayomkosesha usingizi kiongozi huyo. Majuzi Korea Kaskazini na Kusini nusra zirudi tena kwenye medani ya vita baada ya Washington na Seoul kufanya manuva ya pamoja ya kijeshi katika Peninsula ya Korea, jambo lililopingwa vikali na Pyongyang.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO