Rais wa Marekani Barack Obama amewahimiza wabunge wa Congress kuongeza bajeti itakayowezesha kuimarisha usalama katika balozi zake Indianian kote ikiwa ni ishara ya kuwakumbuka raia wanne wa nchi hiyo waliopoteza maisha katika shambulio la mjini Benghazi nchini Libya mwezi Septemba mwaka jana.
Obama amekuja na ombi hilo baada ya wabunge wa Replublicans kuushutumu utawala wake kwa kuficha vielelezo muhimu vya shambulio la Septemba 11 mwaka 2002 wakisema ilikuwa ni ujanja wa kuhakikisha kiongozi huyo anarejea madarakani kwa awamu ya pili katika uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka jana.
Ombi la Obama limekuja siku moja tu baada ya White House kutoa kurasa mia moja za barua pepe na nyaraka zinazoonyesha majibu ya utawala wa Obama juu ya mashambulizi ya mwaka jana katika ubalozi wa Marekani mjini Benghazi.Ikulu ya Marekani ya White House imeomba bunge la Congress kuidhinisha jumla ya dola bilioni 4.4 katika mwaka wa fedha wa sasa ili kuimarisha maswala ya usalama kwa wanadiplomasia wake.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO