Jeshi la Nigeria limetumia helikopta na ndege za kivita katika mapambano yake dhidi ya waasi wa Boko Haram kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Oparesheni hiyo inatekelezwa kufuatia amri ya Rais Goodluck Jonathan wa nchi hiyo ambaye ametangaza hali ya hatari katika ngome za Boko Haram katika majimbo ya Borno, Adamawa na Yobe. Karibu watu 3,500 wamepoteza maisha Nigeria tokea kundi la Boko Haram lianzishe uasi mwaka 2009.
Boko Haram ni kundi lenye misimamo ya kufurutu mipaka nchini Nigeria ambalo kutokana na kuwa na ufahamu mbaya na potofu kuhusiana na Uislamu, limeitumbukiza nchi hiyo katika dimbwi la machafuko na mauaji sambamba na kuzusha hitilafu za kidini na kikabila. Umasikini kwa upande mmoja na upendeleo mkubwa unaofanywa kwa Wakristo dhidi ya Waislamu nchini Nigeria kwa upande wa pili ni moja ya sababu zinazotajwa na wataalamu wa mambo kuwa chanzo cha vijana wa nchi hiyo kujiunga na kundi la Boko Haram.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO