Rais Obama ametetea sera ya matumizi ya ndege zisizokuwa na rubani katika kile alichokiita vita halali.
Katika hotuba muhimu aliyoitoa kwenye chuo kikuu cha ulinzi wa taifa cha Washington, Obama alisema matumizi ya ndege hizo yameifanya Marekani iwe salama zaidi. Hata hivyo amesisitiza kwamba inapasa kuhakikisha kuwa katika matumizi ya ndege hizo hakuna raia anaeudhurika.
Rais Obama pia amesema utawala wake upo tayari kukubali udhibiti zaidi wa mashambulio yanayofanywa na ndege zisizokuwa na rubani, nje ya maeneo ya vita kama Afghanistan. Amesema Marekani ipo vitani dhidi ya kundi ambalo lingewaua Wamarekani wengi kwa kadri ambavyo ingeliwezekana ,laiti hatua zisingelichukuliwa kwanza kulizuia kundi hilo. Juu ya juhudi za kuifunga jela ya Guantanamo, Rais Obama alifahamisha kuwa Marekani imeiondoa hatua ya kuusimamisha kwa muda, mpango wa kuwahamisha wafungwa na kuwapeleka Yemen. Katika hotuba yake kwenye chuo kikuu cha ulinzi wa taifa mjini Washington, Obama aliwaambia Wamarekani kwamba jela ya Guantanamo imegeuka kuwa ishara duniani kote, inayoonyesha jinsi Marekani inavyokiuka sheria.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO