Friday, May 24, 2013

MWANAJESHI ALIYECHINJWA UINGEREZA ATAJWA


Wizara ya ulinzi nchini Uingereza imemtaja mwanajeshi alieuawa mjini London kwa kukatwa visu  na mapanga ,kuwa ni Lee Rigby aleikuwa na umri wa miaka 25 na aliekuwa mwenyeji wa Manchester. Kutokana na habari za kifo cha kutisha cha askari  huyo,kufahamika  zaidi na wananchi, Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ametoa mwito wa kuwepo umoja. Amesema watu waliokifanya kitendo cha mauaji wanajaribu kuwagawanya Waingereza.
Askari alieuawa,Lee Rigby  alijunga na jeshi la  Uingereza mnamo mwaka wa  2006 na alilitumikia  jeshi hilo nchini Cyprus na Afghanistan. Watu wanaotuhumiwa kumuua mwanajeshi huyo ni waingereza wenye asili ya Nigeria ambao sasa wapo kwenye hospitali tofauti chini ya ulinzi wa maafisa wenye silaha.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO